27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KUELEKEA MECHI YA WATANI, Eymael aahidi burudani, ushindi

THERESIA GASPER – DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema anafahamu mechi dhidi ya watani wao wa jadi Simba, itakuwa na ushindani mkubwa, lakini ameahidi kikosi chake kuonyesha kiwango cha kuvutia sambamba na kuibuka na ushindi baada ya dakika 90 kukamilika.

Yanga na Simba zitashuka dimbani Jumapili hii kuumana, katika  pambano mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, litakalopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu hizo zitaumana zikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Januari 4 mwaka huu katika dimba hilo.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Mbao ambao kikosi chake kilishinda mabao 2-0 juzi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Eymael alikiri kuwa wapinzani wake hao wana kikosi imara, lakini akaahidi kuingia na mbinu kali za kuwazuia wasiwe na madhara kisha kusaka ushindi.

“Ushindi katika mechi za hivi karibuni umezidi kutuongezea nguvu kuelekea katika mchezo wetu dhidi ya watani wetu Simba, nafahamu itakuwa ni mechi ngumu ila tumejipanga kuhakikisha tunaonyesha mchezo mzuri na pamoja na kupata ushindi,” alisema Eymael.

Akizungumzia sababu iliyomfanya kutowatumia baadhi ya wachezaji wake muhimu kwenye mchezo dhidi ya Mbao, alisema: “ Niliamua kuwapumzisha baadhi ya wachezaji ili  kuwafanya kuwa fiti zaidi na kuwaepusha na kadi ambazo zingeweza kuwakosesha mechi dhidi ya wapinzani wetu.”

Katika mchezo wa juzi, Eymael hakuwatumia kiungo wake mshambuliaji matata Benard Morrison pamoja na mshambujiaji nyota wa timu hiyo, Ditram Nchimbi.

Eymael alisema ataendelea kuwanoa wachezaji wake na kufanyia kasoro alizozibaini kabla  ya mchezo wao na Simba, ili kuhakikisha wanavuna pointi tatu.

Kocha huyo raia wa Ubelgji aliwataka mashabiki kujitokeze kwa wingi katika mchezo huo, kwani anauhakika wa kuwapata furaha.

Yanga na Simba zinakutana huku Wanajangwani wakiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 47, baada ya kushuka dimbani mara 24 wakishinda michezo 13, sare nane  na kupoteza mara tatu.

Simba kwa upande wake, ipo kileleni  mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 65, baada ya kucheza michezo 25, ikishinda 21, sare mbili na kupoteza mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles