30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KUBENEA: MBUNGE CCM AKIKWAMISHA BAJETI HII NISILIPWE MSHAHARA

Maregesi Paul, Dodoma

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), amesema kama atatokea Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM) akakwamisha bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ataruhusu mshahara wake asilipwe.

Amesema pamoja na kwamba baadhi ya wabunge wa CCM wanaonyesha kutoridhishwa na baadhi ya bajeti za wizara lakini hawana uwezo wa kuzuia bajeti kwa kuwa wanazuiwa na chama chao kufanya hivyo.

Kubenea ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akichangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Katika hatua nyingine kubenea ameliambia bunge kwamba anatarajia kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka bunge liunde kamati maalumu kuchunguza operesheni sangara inavyotekekezwa katika Ziwa Victoria.

“Operesheni hiyo lazima ichunguzwe kwa sababu imeumiza wavuvi na wananchi kwa ujumla,” amesema.

Naye Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM) amesema matatizo yaliyoko nchini yamesababishwa na baadhi ya wataalamu ikiwamo kupiga chapa mifugo huku wakijua wanaharibu ngozi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles