31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kubenea, Komu wahojiwa Kamati Kuu Chadema

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Saed Kubenea (Ubungo) na Anthony Komu (Moshi Vijijini), wamehojiwa na Kamati Kuu ya chama hicho kuhusu ujumbe wa sauti unaodaiwa kuwa ni mazungumzo ya wabunge hao.

Kamati hiyo iliyokutana kwa dharura jijini Dar es Salaam leo Jumanne Oktoba 17, tayari imemhoji Komu kabla ya Kubenea ambaye hadi wakati huu bado anahojiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati kikao hicho kikiendelea, Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, amesema kwa sababu ni kikao cha dharura ajenda ni moja kuhusu mambo ambayo yaliyotokea kwenye mitandao ya kijamii ikiwahusu wabunge hao.

“Wabunge hao walialikwa ili waje waileze kamati kuu kinachoendela kwa sasa tayari Komu ameshahojiwa na Kubenea anaendelea, nipende tu kuwaambia baada ya kikao kumalizika tutatoa taarifa rasmi kuhusu kikao hicho.

“Mamlaka ya nidhamu ni ya kamati kuu kwa hiyo tutakapokamilisha tutatoa taarifa rasmi kwa sasa ni mapema mno kutoa taarifa lakini kamati kuu yetu ni kamati yenye watu weledi tumewapa fursa wabunge hawa kujieleza hiyo clip ilitokea katika mazingira gani na je, ni ya kwao.

“Lakini hiyo clip ukiisikiliza kuna ujinai ndani yake lakini mwisho wa siku kamati kuu itafanya uamuzi wake na uamuzi wowote utakaofanyika utakuwa ndani ya katiba,” amesema Mrema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles