24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kubenea atiwa hatiani kesi ya kumtukana Makonda

KubeneaNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), ametiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kumtukana aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.

Mbali ya kutiwa hatiani, mahakama hiyo imemwachia kwa masharti ya kutotenda kosa la kutoa lugha ya matusi kwa kipindi cha miezi mitatu.

Kubenea alitiwa hatiani na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba juzi.

Hakimu Simba alitoa adhabu hiyo baada ya kuridhika kwamba upande wa Jamhuri umethibitisha kosa bila ya kuacha shaka yoyote.

Akisoma hukumu hiyo alisema wakati wa usikilizwaji upande wa Jamhuri ulileta mashahidi watatu na mshtakiwa alikuwa na mashahidi watatu baada ya kuonekana ana kesi ya kujibu.

Hakimu Simba alisema katika mashauri kama hayo, upande wa Jamhuri ndiyo una jukumu la kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa bila kuacha shaka yoyote na mahakama ijiridhishe lugha iliyotumika ilikuwa ya matusi.

“Baada ya kuchunguza ushahidi wa pande zote mbili, mahakama inaona upande wa Jamhuri umethibitisha kosa, imeonekana ni kweli mshtakiwa alitamka maneno hayo ambayo kwa mazingira yaliyokuwepo yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

“Kutokana na mazingira hayo, mahakama inamtia hatiani mshtakiwa kwa kutumia lugha ya matusi,” alisema Hakimu Simba.

Kabla ya kutolewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, alidai upande wa Jamhuri hauna kumbukumbu za makosa ya nyuma ya mshtakiwa, hivyo aliiomba mahakama itoe adhabu kwa kuzingatia sheria.

Hakimu Simba alifafanua sheria inavyosema kwa makosa kama hayo, akisema adhabu zinazoweza kutolewa kwa mshtakiwa anayetiwa hatiani kwa kosa kama hilo, ni faini au kifungo jela bila ya faini au mahakama inaweza kumwachia bila ya masharti au inaweza kumwachia akae nje kwa masharti.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Simba alimpa nafasi Kubenea kusema lolote ili mahakama iweze kumfikiria katika kutoa adhabu.

u hiyo, mawakili wa Kubenea wakiongozwa na Peter Kibatala, walidai watakata rufani kupinga mshtakiwa kutiwa hatiani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles