24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KUBENEA AKAMATWA DAR

NA CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM


MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), amekamatwa na polisi jijini Dar es Salaam jana ili apelekwe  Dodoma kuhojiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama  ya Bunge.

Hatua hiyo imetokana na agizo lililotolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, mbunge huyo kuhojiwa na kamati hiyo.

Kubenea anatakiwa kuhojiwa baada ya kudai kuwa Spika ameliongopea Bunge kwa kusema risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), ni 30 na tano ndizo zilizompata.

Kubenea alinukuliwa akisema, risasi alizorushiwa Lissu kwenye gari yake ni zaidi ya 30, hivyo Ndugai akaagiza mbunge huyo kuhojiwa na kamati hiyo ili atoe taarifa zaidi.

Jana gazeti hili lilipata taarifa za Kubenea kukamatwa sasa nne asubuhi wakati akijiandaa kwenda Hospitali ya Agha Khan kufanyiwa uchunguzi wa kipimo cha MRI.

Taarifa hizo zilieleza kuwa, baada ya polisi kumkamata na Kubenea kuwaeleza kwamba anasafari ya kwenda hospitali, walioongozana naye hadi Agha Khan.

Baada ya kufanyiwa kipimo hicho mbunge huyo alichukuliwa na polisi na kupelekwa Kituo Kikuu cha polisi kanda ya Dar es Salaam (Central).

Baada ya muda mfupi mbunge huyo alihamishwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay Kinondoni kwa ajili ya taratibu nyingine.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, Kubenea alithibitisha kukamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake.

“Nimewaambia ninaumwa, wakaniambia wao wamepewa taarifa kuwa wanikamate, hawana mamlaka mengine hivyo wanachokifanya ni kunipeleka Dodoma kama walivyoagizwa,”alisema Kubenea.

MTANZANIA lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Mulilo ambaye alisema mzungumzaji wa suala hilo ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Akizungumza kwa njia ya simu na MTANZANIA, Kamanda Mambosasa alisema wamemkamta mbunge huyo kwa hati ya Bunge iliyotolewa na Spika Ndugai.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa hati hiyo inanguvu sawa kisheria na ile inayotolewa na mahakimu au jaji.

“Ni kweli tumemkamata Kubenea na tunategemea kumsafirisha usiku huu (wa jana), ila hadi sasa hatujafahamu kama wataondoka kwa ndege au gari,”alisema Mambosasa.

Hivi karibuni Spika Ndugai aliziagiza  kamati mbili za Bunge,  ziwahoji wabunge  wawili wa upinzani Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo), baada ya kutuhumiwa kutoa kauli zisizofaa dhidi ya Spika Ndugai.

Ndugai aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake, Adad Rajab imuhoji Kubenea  baada ya kukaririwa akiwa katika kanisa moja akizungumzia tukio la kupigwa risasi kwa Lissu.

Pia aliiagiza kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge chini ya Mwenyekiti wake, George Mkuchika kuwahoji wabunge hao.

Ndugai alisema Kubenea anatuhumiwa kutoa tuhuma dhidi ya Spika kuwa amelidanganya Bunge kuhusu idadi chache ya risasi alizopigwa Lissu, kwani ameonekana anajua zaidi tatizo hilo lililomtokea Lissu hivyo akatoe ushahidi ili kusaidia uchunguzi unaondelea.

Kwa upande wake Zitto anatuhumiwa kwamba alimshutumu Spika kuwa amekosea kwenye utaratibu alioutumia katika kushughulikia ripoti mbili za almasi na tanzanite kukabidhiwa serikalini bila kujadiliwa bungeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles