27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kubenea abaini ufisadi Ubungo

Saed KubeneaNA SHABANI MATUTU

MBUNGE wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, amesema fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo hilo zimetafunwa na baadhi ya watendaji wa kata.

Akizungumza katika Kata ya Kimara wakati wa kuhitimisha ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya kata za jimbo hilo, Kubenea, alisema amebaini kuwepo upotevu wa fedha zinazotolewa na Serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya jimbo wenye lengo la kuendesha miradi iliyo katika kata.

Alisema katika Kata ya Kimara amebaini upotevu wa zaidi ya Sh milioni nne na ametaka uchunguzi ufanyike ili wahusika wa upotevu huo wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Aliitumia ziara yake hiyo kutoa msaada wa Sh milioni mbili kwa Kikundi cha Women Group kinachojihusisha na uleaji wa watoto zitakazotumika kununua vyerehani.

Pia alitoa Sh milioni tano katika Kata ya Mabibo kwa ajili ya kununulia matofali yatayotumika kujenga ofisi ya mtaa, Kata ya Makuburi alitoa zaidi ya Sh milioni 10 kwa ajili ya uchimbaji wa kisima na Kata ya Sinza Kontena alitoa Sh milioni 11 kwa ajili ya kusaidia vikundi shirikishi kuendesha miradi yao ya biashara.

“Baada ya kutembelea miradi, nimebaini upotefu wa fedha za Serikali ambazo zilitumwa kusaidia kata kadhaa lakini nyingi hazikuwafikia walengwa.

“Fedha ni za wananchi haiwezekani zipotee hivi hivi lazima zifahamike zimetumikaje na waliozitafuna wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema Kubenea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles