24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kozi za kiarabu na kiiran zaanzishwa nchini

MWANDISHI WETU

KITUO Cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimeanzisha kozi za Kiarabu na kifarsi (Kiiran) kwa wananchi wote wanaohitaji kujifunza lugha hizo.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa kituo hicho, Abbas Farmand  alipokuwa akizungumzia umuhimu wa kujua lugha nyingi ili kurahisisha Mawasiliano.


Alisema waliamua kufanya hivyo ili Watanzania wanaopenda kujua lugha ya kiarabu wachangamkie fursa hiyo na wale wenye mahitaji ya kujua lugha ya Iran pia wajifunze.

“Tumeanza kuwasajili wanaohitaji kupata mafunzo na usajili unatarajia kumalizika Septemba 30 mwaka huu , tunafanyia hapa hapa Kituo cha Utamaduni,”alisema.

Katika hatua nyingine kituo hicho kimeandaa mashindano maalum ya kusherehekea maazazi ya Mtume.


Mkurugenzi Abbas alisema mashindano hayo yako kwa ajili ya mtu yoyote anayetaka kushiriki kuandika mashairi ama makala kuhusu Maisha ya Mtume ama Tabia njema za Mtume.

Alisema mshindi wa kwanza katika shindano hilo atapata zawadi ya Sh 250,000, mshindi wa pili Sh 150,000 na mshindi wa tatu Sh 100,000 na kuongeza kwamba mwisho wa kutuma kazi hizo ni Novemba 10 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles