27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KOREA KUSINI YATAKA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI

SEOUL, KOREA KUSINI


KOREA Kusini imependekeza kufanyika mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini, baada ya majuma kadhaa ya misukosuko, kufuatia hatua ya Korea Kaskazini ya kufanya majaribio ya makombora.

Ikiwa mazungumzo hayo yatafanyika, yatakuwa ndiyo ya kwanza ya juu tangu mwaka 2015.

Maofisa wa vyeo vya juu walisema mazungumzo hayo yatalenga vitendo vyote, ambavyo huchangia kuwapo misukosuko ya kijeshi katika eneo lenye ulinzi mkali kati ya Kusini Kaskazini.

Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in, tangu mwanzo alikuwa ameashiria kuchukua hatua ya kuleta ushirikiano wa karibu na Korea Kaskazini.

Akitoa hotuba hivi majuzi mjini Berlin, Ujerumani, alisema mazungumzo na Korea Kaskazini yanastahili kufanyika na kutaka mwafaka kuafikiwa.

Lakini hatua za Korea Kaskazini kuyafanyia majaribio makombora likiwamo la hivi majuzi la masafa marefu, inaenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa (UN).

Naibu Waziri wa Ulinzi nchini Korea Kusini, Suh Choo-suk, aliuambia mkutano wa wanahabari kuwa mazungumzo yatafanyika eneo la Tongilgak, katika jengo la Korea Kaskazini katika eneo lisilo na ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles