24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

KOREA KUSINI YAIWEKEA VIKWAZO KOREA KASKAZINI

SEOUL, KOREA KUSINI


SERIKALI ya Korea Kusini imetangaza vikwazo vipya dhidi ya mashirika 20 mengine ya Korea Kaskazini, na watu kadhaa, ili kujibu jaribio la kombora na mradi wa nyuklia wa taifa hilo jirani.

Wizara ya Fedha ilisema hatua hizo zinalenga kuzuia fedha kugharamia mradi wa silaha, kinyume cha sheria.

Karibu mashirika na watu hao wote, yamo katika sekta za kibenki na safari za majini, na tayari yamepigwa marufuku na Marekani.

Hatua hiyo inachukuliwa wiki mbili tu baada ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya kufyatua kombora ambalo linasemekana linaweza kufika pahala popote pale nchini Marekani.

Aidha linakuja huku nchi hii, Japan na Marekani zikiwa katika mazoezi ya pamoja, yakiilenga Korea Kaskazini ambayo imekasirishwa na hatua hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles