23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA JAPAN

SEOUL, KOREA KUSINI


JESHI la Korea Kusini limesema Korea Kaskazini imerusha makombora yake kadhaa katika Bahari ya Japan.

Jeshi hilo limesema makombora hayo yamerushwa kutoka kwenye eneo la Tongchang-ri lililo katika mpaka kati ya Korea Kaskazini na China na kurushwa kwa umbali takriban kilomita elfu moja.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe alisema makombora hayo yanadhihirisha ushahidi tosha wa vitisho vipya kutoka Korea Kaskazini

“Korea Kaskazini imefyatua makombora yake manne leo na kuangukia karibu na eneo letu la maji lenye manufaa kwetu kiuchumi,” alisema.

Japan ambayo kwa sasa inakusanya taarifa na kuzichambua kuhusu tukio hili inapinga vikali kitendo cha taifa hilo la kikomunisti kurusha makombora.

Inasema kwamba hilo linaashiria namna Korea Kaskazini ilivyo tishio jipya katika ukanda huo.

“Korea kaskazini ilishatangaza aina hii mpya ya makombora kabla ya kuyarusha leo (jana), hivyo tutafuatilia kwa karibu suala hili kwa umakini mkubwa,” ilisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles