27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Konokono aliyeishi miaka 507 na kuweka historia

konokono
konokono

Na WILLIAM SHAO,

Wanasayansi nchini Uingereza wametangaza kwamba  konokono aliyepatikana nchini Iceland alikuwa na umri wa miaka 507 alipokufa mwaka wa 2006 na si miaka 405 kama ilivyodhaniwa.

Huyo ndiye mnyama aliyeishi muda mrefu zaidi katika historia.

Konokono huyo alikufa wanasayansi walipomgandisha ili wampeleke kwenye maabara.

Tunaposema “mnyama aliyeishi muda mrefu zaidi” katika kisa hiki, jambo hilo halitii ndani vitu vilivyo hai kama vile matumbawe ambayo yanasemekana yamekuwepo kwa maelfu ya miaka.

“Huu ni wakati wa kuandika upya vitabu vya kumbukumbu,” kilisema chanzo kimoja cha taarifa ‘za kuaminika’ za sayansi kinachojulikana kama ‘Science Nordic’.

Katika kipindi cha vuli ya mwaka 2006, timu ya watafiti ilikwenda katika nchi ya Iceland, ambako waligundua kitu ambacho hatimaye kikawa habari kubwa duniani.

Ugunduzi huo uliwekwa pia katika kitabu cha kumbukumbu, ‘Guiness Book of World Records’.

Ugunduzi huo ni wa konokono ambaye awali watafiti walisema alikuwa na umri wa miaka 405, na hivyo akachukuliwa kuwa ni mnyama mkongwe zaidi duniani.

Hata hivyo, baada ya uchunguzi wa kina zaidi, ndipo walipogundua kuwa konokono huyo ana umri mkubwa zaidi kuliko walivyofikiria awali.

“Tulikosea pale mwanzoni, na huenda tuliharakisha mno kuchapisha matokeo ya utafiti wetu. Lakini sasa tuna hakika kabisa tumeupata umri halisi (wa konokono huyo),” alisema mwanasayansi  Paul Butle ambaye ni mtafiti katika Chuo Kikuu Bangor kilichoko Wales nchini Uingereza.

Lakini nini siri ya urefu wa maisha ya konokono huyo? Mtafiti bingwa wa saikolojia ya wanyama, Doris Abele, anaamini hiyo inatokana na mwendo mdogo wa umetaboli, yaani ile hali ya ujenzi na uvunjaji vunjaji wa kemikali mwilini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles