27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

KOMBE LA FA LAANZA NA KIOJA

NA THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM


MICHUANO ya Kombe la Shirikisho(Fa)imeanza na kioja baada ya  mchezo kati ya Prisons na Abajalo uliopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana, kushindwa kufanyika kutokana na baadhi ya wachezaji kukosa leseni.

Kilichosababisha mchezo kukwama kufanyika ni hatua ya baadhi ya  wachezaji wa Abajalo kukosa leseni zinazowaruhusu kushiriki michuano ya Fa.

Miongoni mwa wachezaji 18 wa Abajalo waliofika uwanjani hapo kwaajili ya kipute hicho, saba pekee ndio waliokuwa na leseni.

Akizungumza na Mtanzania, Mwenyekiti wa Abajalo, Edgar Chibura aliliangushia‘jumba bovu’ Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),akisema lilikuwa na taarifa kuhusiana na baadhi ya wachezaji wake kukosa leseni.

 

Alisema kati ya wachezaji wao wapya 11 waliowasajili,watano walitakiwa waanze kwenye mchezo huo.

“Dirisha kubwa la usajili tuliingiza wachezaji 26 kwenye mfumo,lakini baada wengine kuondoka walibaki 11, hivyo tukaamua kusajili wachezaji wengi  dirisha dogo.

 

“Baada ya dirisha dogo kusogezwa mbele nakuambiwa kamati itapitia usajili tarehe 29  tuliwaomba TFF itupe nakala inayoidhinisha wachezaji ili tuweze kuwatumia, lakini hawakufanya,wao ndio wanastaili lawama,”alisema.

Ofisa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema,  timu ya Abajalo itawajibika baada ya kusababisha mchezo huo kutofanyika.

 

 

“Mchezo hauwezi kurudiwa kwakua wao ndiyo  wenye makosa, wasubiri kamati ya mashindano itakachoamua,”alisema.

Naye kamishna mchezo huo, Abdallah Zungo, alisema walihairisha mchezo baada ya kufuata taratibu zote.

“Mimi nitakabidhi ripoti kwa  wahusika,mchezaji anayetakiwa kucheza lazima awe na leseni,”alisema.

 

Kocha Mkuu wa Prisons, Abdallah Mohamed alisema wanasubiri uamuazi wa TFF kuhusiana na jambo hilo.

Katika hatua nyingine mashabiki waliojitokeza kutaka kushuhudia mchezo huo walizua kasheshe baada ya kutaka warudishiwe fedha za viingilio walizolipa kiasi cha Sh 2000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles