27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KOCHA TAIFA STARS: HATUWAACHI BURUNDI

Na MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

KOCHA wa timu ya Taifa Tanzania, ‘Taifa Stars’  Etienne Ndayiragije amesema  hakuna kikwazo kitakachokizuia kikosi chake hicho kuibuka na ushindi kitakaposhuka dimbani leo kuumana na  Burundi ( Intamba m’Urugamba), katika mchezo wa marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2022 nchini Qatar.

Pambano hilo linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa  litapigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza kati ya timu hizo ulipigwa kati kati ya wiki hii jijini Bujumbura, ambapo Stars ililazimisha sare ya bao 1-1.

Ili kusonga mbele hatua ya makundi, Stars italazimisha kusaka sare ya aina yoyote au ushindi, huku wapinzani wao Burundi wakihitaji ushindi pekee ili kupiga hatua nyingine mbele.

Faida iliyonayo Stars kuelekea mchezo huo ni akiba ya bao moja la ugenini ililolipata katika mchezo wa kwanza nchini Burundi.

Kikosi hicho cha Stars kitashuka kuikabili Burundi kikijiamini kutokana na rekodi nzuri inapokutana na timu hiyo nyumbani.

Katika michezo mitano ya mwisho ya timu hizo katika ardhi ya Tanzania, Stars imeshinda mitatu, sare moja na kupoteza mmoja.

Hata hivyo, rekodi za jumla pia zinaibeba Stars inapokuana na Burundi.

Kwa ujumla timu hizo zimekutana mara 19, Stars imeshinda  11, sare tatu na kupoteza mitano.

Mara ya mwisho zilikutana Machi 28, 2017. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Taifa na Stars kushinda mabao 2-1.

Ushindi wa  mwisho wa Burundi dhidi ya Stars iliupata Novemba 28, mwaka 2012.

Katika mchezo huo  wa michuano ya Chalenji ya nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Burundi ilitakata kwa bao 1-0.

Kocha Mkuu wa Stars, Etienne Ndayiragije akizungungumzia maandalizi ya kikosi chake alisema wamejiandaa kiasi cha kutosha kwa ajili ya kuhakikisha wanapata ushindi na kusonga mbele.

Alisema imani aliyonayo inatokana na sehemu kubwa ya kazi waliifanya ugenini hivyo leo watamalizia ungwe iliyobaki kwa kuibuka na ushindi.

“Mchezo wa marudiano utakuwa wa kufa au kupona kwa sababu ndio utakaamua mustakabali wetu, lazima tutumie vema uwanja wetu wa nyumbani  kupata matokeo mazuri na kusonga mbele.

“Kasoro tulizoziaona katika mchezo wa kwanza tumezirekebisha, lakini hata yale mazuri tuliyoana pia tumeyaboresha zaidi mazoezini, vijana wameahidi kukata kiu ya Watanzania kwa kupata ushindi, kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kutupa sapoti,” alisema Mgunda.

Mshambuliaji wa timu hiyo, Simon Msuva ambaye alifunga bao la kusawazisha la Stars kule Burundi alisema kwa upande wao wa wachezaji wamejiandaa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.

“Tunashukuru tulikuwa na mchezo mzuri ugenini, tumerudi nyumbani kwa ajili ya kumaliza kazi, sisi kama wachezaji tuko tayari kujitoa kwa hali yeyote, Huu ni mchezo muhimu kwa Watanzania wote hivyo ni muhimu kuwa na mshikamano ili tufanikishe lengo kwa pamoja,” alisema Msuva.

Naye mshambuliaji Adi Yussuf alisema baada ya kuanza vizuri ugenini watahakikisha wanamaliza kazi nyumbani.


 “ Tulicheza vizuri mchezo wa kwanza ugenini, wachezaji walijituma , tunakila sababu ya kushinda kwani tutakuwa nyumbani huku tukipata sapoti ya Watanzania wenzetu,” alisema mshambuliaji wa  Blackpool ya Ligi Daraja la Kwanza England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles