24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Simba aipa Yanga siri za Township

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amewataka wapinzani wao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kujipanga sawa sawa, akisema Township Rollers si ya mchezo mchezo.

Simba juzi ilicheza mchezo wake wa tatu wa kujipima ubavu ikiwa kambini Afrika Kusini dhidi ya Township na kulazimishwa sare ya bao 1-1.

Wekundu hao wanajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ilicheza mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya  chuo kikuu ya Orbert Tvet na kupata ushindi wa mabao 3-0 , kisha ikaivaa timu ya Daraja la Kwanza ya Afrika Kusini Platinum Stars na kushinda mabao 4-1.

Lakini baada ya sare ya kwanza, Aussems amesema Township ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Botshwana wamempa kipimo kizuri,  baada ya kubaini kasoro kadhaa katika kikosi chake ambazo atalazimika kuzirekebisha kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa  Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba itazindua kampeni zake za Ligi ya Mabingwa kwa kuvaana na US Songo ya Msumbiji, ikianzia ugenini, mchezo utakaocheza kati ya  Agosti 9 na 11.

Kwa upande  mwingine Yanga ambayo pia itaiwakilisha Tanzania  katika Ligi ya Mabingwa Afrika, imepangwa kuanza harakati zake kwa kuumana na Township, mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Agosti 9 na 11, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kabla ya marudio kati ya Agosti 23 na 25, nchini Botswana.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya mtandao Aussems aliisifu Township akisema ni timu imara iliyowapa changamoto uwanjani.

“Mchezo huu umeweza kunipa mwanga mzuri kwa kuendelea kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu niliyoyaona, ukizingatia ni timu kubwa kati ya zote ambazo tayari tumeshacheza nazo.

“Timu hii ni nzuri na inawachezaji wazuri hivyo tunatakiwa kuendelea na mambo mazuri ambayo tayari tumefanya ili kukiweka fiti zaidi kikosi chetu,” alisema na kuongeza.

“Nafahamu Yanga watacheza nayo, sio kwamba hawafungiki lakini ni vizuri wakajipanga sawa sawa kwakua si timu nyepesi hata kidogo.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles