23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Prisons akataa unyonge kwa Yanga

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM


LICHA ya kikosi chake kukamata nafasi za chini  kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohamed, amesema atahakikisha analinda rekodi yake ya msimu uliopita ya kutopoteza pointi tatu dhidi ya  Yanga.

Prisons itakuwa mgeni wa Yanga kesho katika pambano la Ligi Kuu litakalopigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Prisons inakamata nafasi pili katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi 10, sawa na Biashara United iliyoko mkiani kutokana na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Prisons inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, msimu uliopita ilivuna pointi nne katika michezo miwili iliyokutana na Yanga , ikianza kwa sare ya bao 1-1, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Sokoine, katika mchezo wa mzunguko wa pili.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mohamed alisema nafasi yao ya sasa katika Ligi Kuu haiwezi kuwa kigezo cha kupoteza mchezo wao wa kesho, kwani amekiandaa kikosi chake ili kushinda.

“Ni kweli tupo katika nafasi mbaya, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga, tumejipanga ili kushinda na kulinda rekodi yetu ya kupata matokeo mazuri msimu uliopita.

“Tumekuwa na muda kutosha wa kujiandaa, tunataka kutumia uwanja wetu kujiongezea pointi tatu na kujitoa katika nafasi za chini, tunajua wapinzani wetu wana mwendelezo wa kupata ushindi katika michezo mitatu iliyopita, sisi tutawavurugia kwa mara ya kwanza,” alisema Mohamed, kocha huyo bora wa msimu uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles