24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Klopp ampigia debe Van Dijk uchezaji bora

LIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema atahuzunika sana endapo beki wake wa kati, Virgil van Dijk, atakosa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka msimu huu nchini England.

Msimu huu mchezaji huyo anatajwa kuwa beki bora katika michuano hiyo, ambapo hadi sasa Liverpool imefungwa jumla ya mabao 20 katika michezo 34 waliocheza.

Liverpool ipo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu huku wakishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, wakitofautiana kwa pointi moja dhidi ya vinara Manchester City.

“Nitajisikia vibaya sana endapo Van Dijk atakosa tuzo ya mchezaji bora wa msimu huu, naweza kusema msimu huu yeye ni mchezaji ambaye amekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, kipindi hiki kimekuwa tofauti na kilichopita ambapo Kevin De Bruyne na Mohamed Salah walikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu lakini Salah alitwaa tuzo hiyo.

“Tulikuwa na furaha kubwa si kwa sababu De Bruyne aliikosa, kwa kuwa Salah alistahili kwa kiasi kikubwa. Hivyo ninadhani msimu huu hakuna wa kupingana na Virgil kwenye mbio hizo,” alisema kocha huyo.

Kwa sasa Van Dijk ni mmoja kati ya wachezaji sita ambao wanatajwa kuwania tuzo hiyo, wachezaji hao ni pamoja na Raheem Sterling, Sergio Aguero, Bernardo Silva, Eden Hazard na Sadio Mane.

Mpinzani mkubwa katika tuzo hiyo ni pamoja na Sterling ambaye amekuwa na kiwango cha hali ya juu katika kikosi cha Manchester City, hivyo wapo ambao wanaamini Sterling ana nafasi kubwa ya kuchukua tuzo hiyo.

Katika mafanikio ya Manchester City msimu huu yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na kinda huyo wa zamani wa Liverpool, ambaye amekuwa akifunga mabao katika michezo mbalimbali na kuipa pointi tatu timu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles