23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kukutwa na meno ya tembo yenye thamani zaidi ya Milioni 69

KULWA-MZEEDAR ES SALAAM

Jamhuri imewafikisha mahakamani mfanyabiashara, Godlisten Mtui na wenzake wawili  kwa uhujumu uchumi, kukutwa na meno ya tembo yenye thamani zaidi ya  Sh Milioni 69.

Washitakiwa hao wamepanda kizimbani leo Jumanne Mei 21 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde ambapo washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Frank Lucas na Mhando Shomary.

Akisoma mashtaka  Wakili wa Serikali Candid Nasua amedai, washtakiwa hao walitenda kosa hilo Mei 7 mwaka huu, eneo la Mbezi Ruisi jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa washtakiwa wakiwa eneo hilo walikutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh 69,025,000 bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Shtaka lingine la utakatishaji, ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kumiliki vipande hivyo vya meno ya tembo huku wakijua vimetokana na kosa la uwindaji haramu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, hakimu aliwataka washtakiwa hao kutojibu lolote kwakuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), atakavyoelekeza vinginevyo.

Washtakiwa wote wamerudishwa rumande hadi Juni 4 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa kwa kuwa shtaka la utakatishaji linalowakabili halina dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles