25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kubaka mtoto wa miaka 14

DAR  ES SALAAM

MKAZI   wa Kigogo Luhanga, Godfrey Fatal (23), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni,   Dar es Salaam, kwa shitaka la kubaka.

Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, Mwendesha  Mashtaka,  Neema Moshi, alidai Mei 18  eneo la Mabibo,  Dar es Salaam, mshtakiwa alimbaka binti  wa   miaka (14) jina limehifadhiwa.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka hilo na  Hakimu  Kiliwa alisema dhamana iko  wazi kwa masharti  ya  kuwa na wadhamini wawili ambao ni ndugu  wa karibu na  bondi ya Sh 200,000 kila  mmoja.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na alirudishwa rumande hadi Octoba  4 kesi  itakapotajwa tena.

Wakati huohuo, George Constantino(19) na mwenzake, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni kwa shitaka la wizi.

Mwendesha Mashtaka, Ramadhan Mkimbu alidai   mbele ya Hakimu Boniphace Lihamwike, kuwa Desemba 17 mwaka jana eneo la Tandale, washitakiwa  waliiba runinga  ya Samsung  yenye thamani ya Sh 1,400,000, redio ya Sh 750,000 na kisimbuzi chenye thamani ya Sh 99,000.

Vingine walivyodaiwa kuiba ni rimoti na flash vyote vikiwa na thamani ya Sh 15,000 na deki mbili zikiwa na thamani ya Sh 100,000,   mali zote zikiwa na thamani ya Sh 2,364000, mali ya Aziza Kassimu.

Ilidaiwa kuwa kabla na baada ya tukio watuhumiwa walimtishia kwa panga kuweza kujipatia mali hizo.

Washtakiwa walikana kutenda shitaka hilo na walirudishwa rumande hadi Oktoba 3 mwaka huu kesi itakapotajwa  tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles