28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kituo cha mwendokasi Ubungo kuhamishwa

Na Bakari Kimwanga-DAR ES SALAAM

KUTOKANA na kasi ya ujenzi wa Barabara ya Juu Ubungo (Fly Over), serikali kupitia Wakala wa Mabasi Yaendeyo Haraka (DART) imepanga kuhamisha matumizi ya Kituo cha Ubungo Maji  kupisha ujenzi huo.

Akizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki, Mtendaji Mkuu wa DART,  Ronald Lwakatare, alisema   changamoto ya ujenzi huo sasa unalazimu kufanya mabadiliko kwenye kituo hicho.

“Ujenzi was Fly Over ya Ubungo, hasa katika eneo letu la Ubungo Maji sasa tunajitahidi kuhakikisha tunabadili kituo  ili watu wawe salama.

“Tunaelewa ni kituo kinachopendwa na watu wengi nasi kama Dart siku zote tunajali usalama wa watu,” alisema Lwakatare.

MBIA WA PILI

Alipoulizwa mchakato wa kumpa mbia wa pili kwa ajili ya kuendesha  mradi huo wa mabasi ya mwendokasi, Lwakatare, alisema bado  mchakato huo unaendelea.

“Masuala ya ununuzi kwa hiyo tupo mbioni kutafuta mtu atakayeleta huduma ya mabasi na tunaendelea na juhudi za kumpata.

“Tunaamini tutafika mwisho tunajitahidi kuhakikisha kuna mabasi ya kutosha kwa sababu mwitikio umekuwa mkubwa sana,” alisema.

UJENZI NJIA YA MBAGALA

Mtendaji Mkuu huyo wa DART, alisema   kwa sasa taratibu ziko mbioni kukamilika kuhusu mkandarasi wa ujenzi wa   mradi wa Mbagala ambaye  ataanza kazi mwishoni mwa mwaka huu.

“Mungu akipenda mwishoni mwa mwaka huu mkandarasi huenda akawa site (eneo la ujenzi) kwa njia ya Mbagala. Tunawaomba na tunawashukuru  wananchi kwa kuupokea vizuri mradi huu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles