30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KITABU APP: TEKNOLOJIA YA KISASA INAYOHAMASISHA KUSOMA VITABU

 Na Mwandishi Wetu


“NAFIKIRI tunatakiwa  tujitahidi  kuibua wananchi wanaosoma. Ni ukweli ambao tunapaswa tuutambue, katika kuhangaika na dunia  ya kisasa, watoto barani Ulaya  wana bahati mbili kubwa  wakilinganishwa na wa kwetu.

“Moja   ni kwamba wana mazoea na vitu vinavyotumia mashine; nyingine  na ambalo ni muhimu zaidi wanayo mazoea na vitabu. Kwa bahati mbaya katika jamii yetu kwamba mtu akionekana amekaa akijisomea  tunamtuhumu kwamba ni mvivu au anapenda kujitenga  na jamii. Tabii hii lazima tuibadilishe,” hii ilikuwa ni kauli ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa jijini Arusha Novemba 29, 1965.

Shuleni  kuna watu wenye tabia ya kujisomea  tu nyakati mitihani inapokaribia  lakini baada ya hapo  vitabu huwekwa mbali.

Takwimu za Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) zinaonesha kuwa wastani wa kujisomea miongoni mwa Waisraeli ni asilimia 64 kwa mwaka, Wajapan asilimia 40, Wamarekani asilimia 21 wakati Wafaransa ni asilimia 20. Ikilinganishwa na Watanzania ni asilimia ndogo wanaomiliki maktaba zao wenyewe, lakini kwa upande wa vijana ni kama hilo halipo.

Kujisomea si tu kwamba kuna faida kwa wasomaji  kwa mkondo wa moja kwa moja, bali pia ni jambo ambalo  kizazi kijacho kinatakiwa kiwe nalo.

Tabia ya kawaida ya kujisomea  duniani kote inapotea hususani hivi sasa  ambapo vifaa vya kielektroniki vinafanya iwe rahisi  kuzipata taarifa kupitia mtandao wa intaneti.

Kutokana na hali hiyo sehemu kubwa ya Watanzania  wanakosa taarifa nyingi za msingi zilizo na manufaa  kiuchumi na kijamii.

Tigo na Kitabu App

Hata hivyo yamekuwapo maendeleo mapya  kwani Tigo Tanzania  hivi karibuni ilizindua vitabu –elektroniki (e-books).

Mfumo huu unatoa aina mbalimbali za vitabu ambapo msomaji anaweza kuarifiwa  kipi akisome. Meneja wa Mawasiliano ya Tigo, Woinde Shiasel anasema kampuni hiyo itaendelea  kuhakikisha kuwa  utamaduni wa kujisomea  unarudi. Tigo inaamini kuwa  jukwaa hili litaamsha utamaduni wa kujisomea miongoni mwa wanajamii  na hivyo kuurudisha utamaduni wa kujisomea ambao ulikuwa umetoweka. Hakuna shaka kwamba kila Mtanzania ataitumia simu yake ya mkononi  kwa manufaa kupitia kujisomea.

“Wateja wetu wengi  hivi sasa wanapenda kutumia simu za kuchati na marafiki na wanafamilia,” alibainisha Shisael na kuongeza; “Kupitia Kitabu App tunawapatia jukwaa sahihi kwa waandishi, waelekezaji na wasomaji kwa ujumla  sehemu ambayo  wanaweza kusoma kwa urahisi mada mbalimbali kupitia simu za mkononi.”

Kitabu App, imeingia katika soko ikiwa  ni suluhisho si tu kwa wasomaji bali pia kwa waandishi ambao hivi sasa wanaweza kuuza  na kufuatilia mauzo ya vitabu vyao kupitia simu zao za mkononi, kwa kutumia mtandao wa Tigo 4G LTE ambao ni mtandao mkubwa wa kasi na mpana uliounganishwa nchini.

Kuwapo kwa vitabu vinavyojieleza kwa sauti  katika jukwaa hilo moja, zana hii inatarajiwa kubadilisha  namna ambavyo Watanzania wanavyoipokea hali ya kujisomea dhidi ya kushuka  ambako kwa kiwango kikubwa  kunahusiana na  utamaduni duni wa kujisomea,” anaelezea Shisael.

Akitoa maoni yake kuhusu zana hiyo, Mkurugenzi wa Jackson Group, Kelvin Twissa anasema; “Zana yetu ya Kitabu App ni ubunifu uliochochewa na mkakati, kulikohamasishwa na  kukua kwa teknolojia jumuishi. Kupitia zana hii  tunaruhusu waandishi kufikia  viwango vya juu vya usomaji kupitia  simu zao za kisasa. Wakati tuna waandishi wengi walio na vipaji katika aina tofauti za vitabu , pia kuna hitaji kubwa la uelewa kwa mapana.

“Tunaamini kwa kuingiza mada  nyingi katika katalojia (Catalogue) yetu inayokua  tunaweza kuleta mapinduzi katika usambazaji wa mada ndani ya nchi na hivyo kuleta hamasa ya kujisomea kwa Watanzania.”

 Twissa aliongeza, “Kitabu App ni zana ya kuelimisha, kuburudisha na kuunganishwa na mada za kidini. Elimu ni moja ya mtazamo wetu wa msingi, hivyo tunajenga  ushirikiano na kutoa wito kwa taasisi za kielimu  kupakua mada zao, hivyo kuokoa gharama za kuchapisha  na hata usambazaji wa vitabu”.

Kitabu App ni zana inayopakuliwa bure;  hivi sasa na inapatikana  kupitia simu za Android  ambapo mtumiaji  anatakiwa kulipia mada inayotakiwa na mtu binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles