KISA GIGI HADID, ZAYN AUZA NYUMBA

0
937

LONDON, UINGEREZAMWIMBAJI maarufu wa muziki nchini Uingereza, Zayn Malik, ametangaza kuuza nyumba yake iliyopo Kaskazini mwa Uingereza na kuhamia Jiji la New York nchini Marekani, kwa ajili ya kumfuata mpenzi wake, Gigi Hadid.

Nyumba hiyo inasemekana ina vyumba vitano vya kulala, lakini ameamua kuiweka sokoni ili kwenda kuishi pamoja na mrembo huyo raia wa Marekani.

Zayn mwenye miaka 25, alikaa miezi 12 jijini New York na mrembo huyo, hivyo ameamua kufanya maamuzi ya kutaka kuhamia moja kwa moja nchini humo baada ya uhusiano wa wawili hao kuendelea kushamiri kwa kasi.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa Zayn amekuwa na furaha sana kuishi nchini Marekani kwa sasa na anaamini huu ni muda sahihi wa kuuza nyumba hiyo na kukimbilia Marekani anakotumia muda mwingi kuishi.

Thamani ya nyumba hiyo imetajwa kuwa pauni milioni 3.5 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni nane za Kitanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here