27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kipa Liverpool aichukulia hatua Besiktas

ISTANBUL, UTURUKI

MLINDA mlango wa Liverpool, Loris Karius, ameichukulia hatua za kisheria klabu ya Besiktas kwa kushindwa kumlipa posho zake ikiwa anaitumikia timu hiyo kwa mkopo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akiitumikia timu hiyo tangu Agosti 2018, aliondoka Liverpool baada ya klabu hiyo kufanikiwa kuinasa saini ya Alisson Becker kutoka AS Roma.

Inasemekana kuwa mchezaji huyo anaidai klabu hiyo zaidi ya Euro milioni 1 kutokana na kutolipwa kwa kipindi cha miezi minne, hivyo ameamua kuchukua hatua kwa kwenda kuishtaki klabu hiyo katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtandao wa Goal, mchezaji huyo alianza kupeleka malalamiko yake FIFA tangu Februari 20, mwaka huu, huku barua hiyo akitaka alipwe kilicho chake mapema iwezekanavyo.

FIFA walichukua hatua mapema iwezekanavyo na kuitaka klabu hiyo ihakikishe inamalizana na mchezaji huyo ndani ya siku 10 tangu kupata kwa barua hiyo, lakini inasemekana kwamba hadi sasa Besiktas haijafanya lolote kwa mchezaji huyo.

Katika msimamo wa ligi nchini Uturuki, klabu hiyo inashika nafasi ya tatu, huku ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya michezo 25, wakati huo nafasi ya kwanza ikiongozwa na Istanbul Basaksehir ikiwa na pointi 57, wakati huo Galatasaray ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 49.

Hadi sasa imesalia michezo nane kumalizika kwa msimu huu, hivyo Besiktas inapambana kuhakikisha inabaki katika nafasi nne za juu.

Karius tangu amejiunga na klabu hiyo akitokea Liverpool, amecheza jumla ya michezo 26 ya michuano mbalimbali, huku mkataba wake wa mkopo ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2019-20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles