30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KIONGOZI WA UPINZANI ZAMBIA KUACHIWA LEO

LUSAKA, ZAMBIA

SERIKALI ya Zambia leo imepanga kuifuta kesi ya uhaini inayomkabili Kiongozi wa upinzani nchini hapa, Hakainde Hichilema na kumwachia huru kutoka jela.

Ni kufuatia maafikiano na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland na wanasheria wengine.

Hichilema, ambaye ni kiongozi wa chama cha Umoja wa Maendeleo ya Taifa (UPND) pamoja na wengine watano walikamatwa Aprili mwaka huu.

Walifunguliwa mashitaka ya uhaini baada ya msafara wa magari ya Hichilema kugoma kuupisha ule wa Rais Edgar Lungu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland aliyezuru Zambia wiki iliyopita aliwaambia wanahabari kuwa pande zote mbili zimekubali ofisi yake iongoze mazungumzo kati yao.

Kesi dhidi ya Hichilema inapaswa kuanza, lakini vyanzo viwili vya habari vimesema mwendesha mashtaka atawasilisha ombi la kesi hiyo kutupiliwa mbali.

Kesi hiyo imezusha taharuki za kisiasa katika nchi hiyo inayozalisha shaba na inayotazamwa kama kati ya nchi thabiti za Afrika na zinazokuza demokrasia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles