33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongozi Iran ahutubia, alitetea jeshi kudungua ndege

TEHRAN, IRAN

KIONGOZI wa kidini wa Iran, Ayatollah Khamenei  jana alijitokeza kuhutubia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 huku akilitetea jeshi la nchi hiyo  baada ya kukiri kudungua ndege ya abiria ya Ukraine kimakosa.

Kiongozi huyo wa juu wa kiroho aliongoza sala ya Ijumaa katika msikiti wa Mosalla mjini Tehran hatua ambayo imekuja wakati ambao kuna wimbi la maandamano ya watu wenye hasira baada ya kudunguliwa kwa ndege hiyo iliyokuwa na abiria 176.

Alisema jeshi hilo maarufu kama ‘Revolutionary Guard’ lilikuwa likiimarisha ulinzi wa Iran.

Kiongozi huyo ametoa rai ya kuwapo kwa umoja wa kitaifa  na kusema kuwa maadui wa Iran ndio msingi wa kudunguliwa kwa ndege hiyo kutokana na mauaji ya kiongozi wao wa juu wa kijeshi, Qasem Soleimani.

Tukio la kudungua ndege linadaiwa kutekelezwa kimakosa wakati wanajeshi wa Iran wakilipa kisasi dhidi ya Marekani iliyomuua kiongozi wao huyo wa juu wa kijeshi kwa maagizo ya Rais wa Marekani Donald Trump. 

Utawala wa Iran pia uko kwenye shinikizo kutokana na kuporomoka kwa uchumi hali iliyosababishwa na vikwazo vya Marekani.

Siku ya Jumatano, Rais Hassan Rouhani aliomba kuwepo kwa mshikamano wa kitaifa.

Lakini katika ishara ambazo hujitokeza kwa nadra ndani ya utawala wa Iran, rais Rouhani amelitaka jeshi kuwajibika kwa kutoa maelezo ni kwa vipi waliidungua ndege ya Ukraine.

Ndege aina ya Boeing 737-800, iliyokuwa ikisafiri kwenda Kyiv ikiwa na abiria wengi waliokuwa wakielekea Canada, iliangukamuda mfupi baada ya kupaa kutoka Tehran, tukio lililogharimu maisha ya watu 176 waliokuwa kwenye ndege.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles