24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongera, Majwega ‘out’ Simba v Azam

kiongeraNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

TIMU ya Simba huenda ikashindwa kuwatumia nyota wake wapya iliyowasajili usajili wa dirisha dogo kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Azam kesho, kutokana na kubanwa na taratibu za usajili nchini.

Baadhi ya wachezaji hao iliyowasajili ni mshambuliaji Paul Kiongera waliyemrudisha kwa mkopo akitokea KCB ya Kenya, winga Brian Majwega kutoka Azam FC, straika kinda Hijja Ugando.

Wengine ni beki Novatus Lufunga aliyetokea African Sports pamoja na mshambuliaji Danny Lyanga aliyetokea FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Habari zilizolifikia MTANZANIA jana zimedai kuwa si wachezaji hao tu wa Simba watakaoshindwa kucheza, bali ni wote waliosajiliwa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

“Hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kucheza bila Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia usajili wote pale dirisha la usajili litakapofungwa Desemba 15 mwaka huu, kama ilivyo kawaida na wale watakaopita watapewa leseni za kucheza,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilieleza kuwa hakuna mchezaji yeyote wa kigeni aliyesajili dirisha dogo, atakayeruhusiwa kucheza kama klabu yake haijamlipia Dola za Marekani 2,000 (zaidi ya Sh milioni 4 za Kitanzania), ili kupata leseni ya kucheza kwa mujibu wa sheria mpya za TFF.

Simba ilikuwa inategemea sana usajili huo mpya ili kuweza kufanya vizuri dhidi ya vinara Azam FC wenye pointi 25, hivyo kuwakosa litakuwa pigo kubwa kwa upande wao kuelekea mchezo huo.

Wachezaji hao wote wameonekana kufanya vizuri sana kwenye kambi ya Simba visiwani Zanzibar, hali ambayo ilikuwa inawapa nguvu wekundu hao kufanya vizuri katika mchezo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles