27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KINA MDEE KUWABURUZA KORTINI SPIKA NDUGAI, MKUCHIKA

         Spika wa Bunge, Job Ndugai

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee, John Mnyika (Kibamba) na Ester Bulaya (Bunda), wamepeleka ombi Mahakama  Kuu Kanda ya Dodoma, kuomba kumshtaki Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika.

Wabunge hao kwa pamoja wanataka kufungua kesi hiyo kutokana na kutoridhishwa na adhabu zilizotolewa kwao, wakidai ni kinyume na kanuni za Bunge.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Kambi ya Upinzani Bungeni imepata taarifa ya kutaka kukamatwa kwa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche kutokana na kuwataka wananchi walinde rasilimali zao baada ya Rais kusema Mgodi wa Acacia hauna kibali cha kuchimba dhahabu nchini.

Alisema wameamua kupeleka maombi Mahakama Kuu kuomba kumshtaki Spika Ndugai na Mkuchika kupinga uamuzi wa kusimamishwa kutohudhuria vikao.

“Hawa viongozi wetu watatu wamepeleka maombi ili Mahakama Kuu iweze kutoa amri ya kufutilia mbali uamuzi wa Spika wa Bunge letu, wa kumsimamisha Mheshimiwa John Mnyika kwa vikao saba vya Bunge hili la saba.’

“Pia Mahakama Kuu iweze kufuta kabisa uamuzi wa Bunge wa kuwasimamisha kuhudhuria vikao vilivyobaki vya Bunge hili, vikao vyote vya Bunge la nane na vikao vyote vya Bunge la tisa walivyowasimamisha Halima Mdee na Ester Bulaya,’’ alisema.

Aidha sababu nyingine alisema hoja ya uamuzi wa Spika ilikuwa na upendeleo kwa kuwanyima haki wabunge wa upinzani na kuwapendelea wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Spika kwa maneno aliyoyasema bungeni kwamba hawa waheshimiwa siku ya Jumatatu ni adhabu tu, Spika huyo huyo siku ya Jumatatu akawa ndio jaji wa hilo shauri, huwezi kuwa jaji katika shauri lako mwenyewe, inaonyesha dhahiri kulikuwa na upendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles