24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kina Kitilya, Masamaki, wapigwa kalenda kortini

masamaki

Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna wa Kodi na Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki na wenzake, hadi Agosti 23 mwaka huu.

Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa alidai  mbele ya  Hakimu, Huruma Shahidi, kuwa upande wa Jamhuri  haujakamilisha upelelezi na kuiomba mahakama  kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Shahidi aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 23 mwaka huu itakapotajwa tena.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Haroun Mpande wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA, Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha  ICD Azam, Eliachi  Mrema ,  Mchambuzi  Mwandamizi  wa Masuala ya Biashara  TRA,  Hamis Omary , Meneja wa Oparesheni  za Usalama na Ulinzi  ICD, Raymond Adolf Louis  na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan .

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa likiwamo la kudaiwa kuwa kati  ya Juni Mosi na  Novemba 17, 2015 walikula njama kwa kuidanganya Serikali.

Wanadaiwa kudanganya kuwa makontena 329  yaliyokuwapo katika Bandari Kavu ya Azam (AICD) yalitolewa baada ya kodi zote kufanyika wakati haikuwa  kweli.

Katika kesi nyingine, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeshindwa kusikiliza rufaa ya Mkurugenzi wa Mshitaka (DPP) dhidi ya aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya na wenzake, kwa vile mawakili wa washitakiwa hao kutofika mahakamani.

Katika rufaa hiyo, DPP anapinga uamuzi wa washitakiwa hao kufutiwa shtaka la nane la utakatishaji fedha uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchaulu.

Shauri hilo lilifikishwa  mahakamani hapo jana mbele ya Jaji Edson Mkasimongwa.

Wakili wa Utetezi, Dk. Masumbuko Lamwai alidai  mawakili wawili wa upande wa utetezi walishindwa kufika mahakamani hapo kutokana na udhuru.

Mawakili hao ni Alex Mgongolwa ambaye  ni mgonjwa na Majula Magafu ambaye alikuwa na kesi nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles