30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KIM JONG-UN AKUTANA NA UJUMBE WA KOREA KUSINI


SEOUL, KOREA KUSINI   |   

KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amewaandalia mkutano na chakula cha jioni wajumbe wawili kutoka Korea Kusini, ikiwa ni mara ya kwanza kiongozi huyo kukutana na ujumbe kama huo tangu aingie madarakani mwaka 2011.

Shirika la Habari la Korea Kusini la Yonhap, liliripoti kuhusu mkutano huo likimnukuu msemaji wa rais wa Korea Kusini.

Ujumbe huo uko Korea Kaskazini kwa mazungumzo yasiyo ya kawaida yenye lengo la kuanzisha mchakato kati ya Korea Kaskazini na Marekani.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeboreka baada ya mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi.

Ujumbe huo unawajumuisha maofisa wenye vyeo vya uwaziri akiwamo Mkuu wa Ujasusi, Suh Hoon na Mshauri wa Usalama, Chung Eui-yong.

Awali, Chung aliwaambia   waandishi wa habari kuwa atawasilisha azimio la Rais Moon Jae-in la kudumisha mazungumzo na kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo na kuondoa silaha za nyuklia kutoka Rasi wa Korea.

Rais wa Marekani, Donald Trump, alisema juzi kuwa Marekani itakuwa tayari kukutana na Korea Kaskazini lakini akasisitiza   Korea ni lazima iondoe zana zake za nyuklia.

Hata hivyo Korea Kaskazini ambayo imesema inataka kufanya mazungumzo na Marekani, imesema kuwa ni hatua ya ‘kishenzi’ kwa Marekani kuweka masharti.

Mwisho

 

‘Italia yajikuta wakati mgumu kuunda serikali’

ROME, ITALIA

MATOKEO ya awali ya Uchaguzi Mkuu   yaliyotolewa jana yanaonyesha vyama vitalazimisha kuwa na mazungumzo magumu na marefu ya kuunda serikali kutokana kukosekana kwa mshindi mwenye wingi wa kutosha Bungeni,

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Italia, muungano unaofuata siasa za wastani za mrengo wa kulia, unaongozwa na Waziri Mkuu wa zamani, Silvio Berluscon, unaongoza kwa asilimia 37.

Muungano huo unahusisha chama chake cha Forza Italia, chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, Liga Nord na chama cha Ndugu wa Italia.

Hata hivyo, Liga Nord, kinachoongozwa na Matteo Salvini kimejipatia asilimia 18 ya kura na kukipita chama cha Berlusconi kilichopata chini ya asilimia 14.

Muungano huo unafuatiwa kwa karibu na Vuguvugu la Nyota Tano (M5S) lilichojipatia asilimia 31 ya kura.

Berlusconi alitarajia chama chake kingejipatia wingi   kura nyingi kuliko washirika wake.

Matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa jana asubuhi yanaashiria juhudi za kuundwa serikali imara zitakuwa tete na zitadumu muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles