25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kilio uhaba wa damu Moi chasikika

Na AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM 

TAASISI ya Mifupa (Moi), imekusanya zaidi ya uniti 1,000 za damu katika kambi iliyofanyika jana Dar es Salaam.

Damu hiyo imekusanywa baada wanachama wa Taasisi ya Familia ya Amani Duniani (FFWPU) kujitokeza kuchangia, ikiwa ni siku chache tangu Moi kutangaza kuhitaji damu kutoka kwa wadau ili kuiwezesha kufanya vyema shughuli zake.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa Moi, Patrick Mvungi, alisema taasisi hiyo ina uhitaji mkubwa  wa damu kwa watu wanaohitaji kufanyiwa upasuaji.

“Tulishirikiana na shirika hili kutoa hamasa kwa wananchi na wamejitokeza kwa kiwango kikubwa, na idadi hii haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa taasisi hii,” alisema Mvungi.

Alisema katika utoaji wa huduma zao za kila siku, wamejipanga kwa kiwango kikubwa, lakini changamoto inayowakabili ni upatikanaji wa damu.

“Hakuna mgonjwa aliyewahi kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa damu, tuna utaratibu wa kuwahudumia wagonjwa na tunahakikisha upatikanaji wa damu katika taasisi, matumizi yetu kwa siku ni chupa 16,” alisema Mvungi.

Kwa upande wake, Kiongozi Mkuu wa FFWPU, Staylos Simba, alisema waliamua kuonyesha moyo huo wa kuhamasisha wanachama kujitolea damu kutokana na changamoto ya damu iliyotangazwa na taasisi hiyo.

“Baada ya kuonana na uongozi wa Moi, niliwaahidi kuwa wanachama wetu zaidi ya 1,000 kutoka Mbagala watakuja kuchangia damu,“ alisema Mvungi.

Alisema hamasa hiyo ya wananchi imetokana na elimu waliyoitoa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutoa damu.

“Leo wanachama wetu kutoka Mbagala wamekuja, lakini tuna wanachama wengi kutoka maeneo mengi watakuja kuchangia damu ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika uimarishaji wa huduma za afya, pia wanachama wetu wengine wataenda kutoa huduma zingine za afya Morogoro,” alisema Mvungi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles