25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

KIKWETE ATAKA TEKNOLOJIA IWAFIKIE WAKULIMA, WAFUGAJI

NA MWANDISHI WETU

-MOROGORO

RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete, ametaka teknolojia mpya ya kilimo, ufugaji na uvuvi inayoonyeshwa wakati wa maonyesho ya wakulima na wafugaji maarufu kama Nanenane, iwafikie wananchi ili kuwakwamua katika umasikini.

Kauli hiyo aliitoa juzi baada ya kutembelea vipando na mabanda katika maonesho hayo Kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere mjini Morogoro.

Alisema pamoja na wataalamu wa sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi kujitahidi kuvumbua teknolojia mpya katika sekta hiyo, bado haiwafikii wananchi wa vijijini.

Hivyo amewataka watalaamu hao pamoja na kuongeza jitihada za kuvumbua, elimu hiyo waipeleke kwa wananchi ili kuondoa umasikini miongoni mwao.

“Kazi kubwa imefanyika ya utafiti, viwango vimeongezeka sana vya ubora, suala kubwa ni namna gani uvumbuzi unaofanywa na maabara kwenye vituo vyetu utawafikia wakulima,” alisema Kikwete.

 

Alisema ili kuondokana na umasikini kwa haraka, wataalamu wanatakiwa kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji namna ya kulima na kufuga kibiashara na kuondokana na dhana ya kufanya kazi hizo kwa kujikimu peke yake.

Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles