30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KIKOSI CHA YANGA CHATUA BOTSWANA, CHATAMBA

Theresia Gasper -Dar es salaam

KIKOSI cha Yanga, tayari kimewasili nchini Botswana tayari kwa mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers, unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi.

Yanga katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, walilazimishwa sare ya bao 1-1 hivyo kuhitaji ushindi au sare ya zaidi ya mabao 2-2 ugenini ili kusonga mbele.

Wachezaji waliopo katika msafara wa kikosi cha Yanga ni Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili, Kelvin Yondan, Paul Godfrey ‘Boxer’, Muharami Issa ‘Marcelo’, Ally Mtoni ‘Sonso’, Deus Kaseke, Mrisho Ngassa, Mapinduzi Balama, Mohamed Issa ‘Mo Banka’ na Feisal Salum.

Wengine ni Papy Tshishimbi, Lamine Moro, Sadney Urikhob, Juma Balinya, Patrick Sibomana, Maybin Kalengo na Issa Bigirimana. 

Wachezaji waliobaki nchini ni Farouk Shikalo, Mustapha Seleman na David Molinga kwa sababu mpaka sasa bado hawajapata leseni zao kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Akizungumza na MTANZANIA jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kikosi hicho kiliondoka alfajiri nchini na kuwasili Afrika Kusini saa nne asubuhi.

“Wachezaji wamefika asubuhi hii Afrika Kusini salama na jioni kwenye saa 11, wataingia Gaborone (Botswana) tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Township,” alisema.

Alisema yeye alitangulia mapema nchini Botswana kuweka kila kitu sawa kabla ya timu yao haijatua huko.

Mwakalebela alisema kwa maandalizi waliyofanya, lazima watoke uwanjani na pointi zote tatu muhimu na kutinga hatua inayofuata.

“Tulipata sare nyumbani, lakini nilikuja huku mapema kuandaa mazingira, vilevile tumeshakiweka sawa kikosi chetu kuhakikisha hatufanyi makosa kwenye mchezo wetu wa marudiano,” alisema.

Yanga imepania kupata ushindi ugenini, licha ya sare waliyopata nyumbani, ili waweze kusonga mbele katika michuano hiyo ya Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles