30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KIIR, MACHAR WASAINI MKATABA KUGAWANA MADARAKA SUDAN

JUBA, SUDAN KUSINI


SERIKALI ya Sudan Kusini na kundi la upinzani wametia saini mkataba wa kugawana madaraka, kama moja ya njia ya kuleta amani nchini hapa.

Rais Salva Kiir na kiongozi wa upinzani, Riek Machar wa PLM-IO, wamekuwa wakizozana kwa muda mrefu.

Sudan Kusini ilipata uhuru wake mwaka 2011 ambao viongozi hao walishirikiana kuutafuta.

Aidha, waliunda Serikali ya Mseto, Kiir akiwa rais na Machar, makamu wa rais lakini mwaka 2013, baada ya Machar kupigwa kufukuzwa kwenye wadhfa wake, mgogoro uliibuka.

Baada ya kuibuka kwa mgogoro huo, makundi yanayomuunga mkono Machar na Rais Kiir, yaliingia vitani na kusababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu kugeuka wakimbizi.

Hata hivyo, taarifa kutoka nchini humo zimeeleza kuwa Jumatano wiki hii, wawili hao walitia saini mkataba wa kugawana madaraka katika mazungumzo yaliyofanyika mjini Khartoum, Sudan.

Awali, makubaliano hayo yalifikiwa mapema Julai, mwaka huu nchini Uganda ambapo serikali mpya itakayobuniwa itakuwa na nyadhifa 35.

Serikali ya sasa ya Kiir itakabidhiwa nafasi 20 za mawaziri huku Machar akipewa  mawaziri tisa na nafasi zitakazosalia zitachukuliwa na makundi mengine ya upinzani.

“Rais Kiir na Machar watatia rasmi saini mkataba huo Agosti 5, ili kuunda Serikali mpya licha ya makundi husika kusaini leo (jana) makubaliano ya awali,” alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Al-Dirdiri Mohamed Ahmed.

Hata hivyo, makundi madogo ya upinzani yalikataa kutia saini mkataba huo yakidai haujaeleweka vyema.

“Mkataba huo hauweki wazi iwapo Serikali ya sasa itavunjwa au kuiongeza ili kujumuisha utawala wa kila kundi,” ilieleza taarifa ya kundi la SPLM iliyotumwa katika vyombo vya habari jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles