26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kigogo CUF ahamia CCM

ALLAN VICENT

Mwanachama Mkongwe wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Singo Kata ya Gongoni katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Mkoani hapa, Hamisi Mwanri (53) amekihama chama hicho na kujiunga CCM.

Mwami ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo kwa miaka 20 sasa amesema kuwa ameamua kuhamia CCM kwa utashi wake mwenyewe baada ya kusoma alama za nyakati na kuridhika na utendaji wa Rais John Magufuli.

Amebainisha kuwa akiwa Mwenyekiti wa mtaa huo chini ya CUF aliweza kusimamia vema miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo mratadi wa wa TASAF (II) wa ujenzi wa barabara wenye thamani ya Sh. milioni 42 mwaka 2008-2009 ikiwemo mradi wa ufugaji kuku wa kikundi cha walemavu wenye thamani ya Sh. milioni 28 na miradi yote ya TASAF (III).

Aidha amesema uroho wa madaraka unaokitafuna chama cha CUF na vyama vingine vya upinzani ni miongoni mwa mambo ambayo yamedhoofisha upinzani hapa nchini na hivyo kushindwa kuwa watetezi wa wananchi,  ndiyo maana ameamua kujiunga na timu ya watu makini wanaojali sana maslahi ya wananchi.

Mwami amepinga wanaodai kuwa amenunuliwa na CCM akihoji kwa nini hawakudai amenunuliwa na CUF kipindi alipojiunga nao ambapo alisisitiza kuwa aliingia na kuondoka kwa utashi wake na hivi sasa ameamua kuingia CCM kwa utashi wake pasipo kushawishiwa na mtu.

“Nimesoma alama za nyakati, upinzani hauna la kusema sasa hivi ndio maana nimeamua kuhamia CCM kwa utashi wangu na sio kwa kununuliwa au kushawishiwa na mtu kwani nina uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika siasa sasa nimekuwa kiongozi wa Serikali hivyo nina upeo wa kuona mbali”, amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles