23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kigamboni International Marathon kurindima Desemba 2

      Bethsheba Wambura, Dar es Salaam



Katika kuadhimisha siku ya Siku ya Ukimwi duniani, Kampuni ya E World imeandaa mashindano ya riadha (Kigamboni International Marathon), itakayofanyika jijini Dar es Salaam Desemba 2, mwaka huu.

Lengo la mashindano hayo ni kuijengea jamii uelewa na hamasa juu ya umuhimu wa kutunza afya na kufanya mazoezi na kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuhamasisha Watanzania kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano Oktoba 24, Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Riadha na Makamu Mwenyekiti Shirikisho la Michezo ya Riadha ya Walemavu nchini, Dimo Mtiki, amesema wanakusudia kuchochea shughuli za kiuchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji, biashara na vivutio vya kitalii vilivyopo Kigamboni na kuimarisha afya na kuhamasisha michezo ya riadha kwa maendeleo ya taifa.

“Kwa siku za hivi karibuni, tumeshuhudia viongozi wetu wakihamasisha wafanyabiashara na wadau mbalimbali kuwekeza ndani ya wilaya yetu ya mpya ya Kigamboni hivyo ni imani yetu kuwa kufanyika kwa Kigamboni International Marathon kutawavutia watu mbalimbali na kujionea uzuri na fursa zilizopo hapa.

“Mashindano haya yatafanyika katika sehemu yenye mandhari nzuri na ya kipekee ya Fun City, ili kutoa nafasi kwa washiriki kuburudika na michezo mbalimbali ikiwemo kuogelea baada ya mbio hizo,” amesema.

Amesema katika mbio hizo, kutakuwa na mbio za urefu wa Kilomita 21(half marathoni), mbio kwa ajili ya watoto na wazee na medali za Dhahabu na Shaba na pesa taslimu zitatolewa kwa washindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles