31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kifo cha mtu mweusi chaibua vurugu

WASHINGTON, MAREKANI

KUMEKUWA na vurugu na mapambano kati ya polisi na waandamanaji katika mji wa Minneapolis nchini Marekani, baada ya kifo cha mwanaume mmoja mweusi akiwa mikononi mwa polisi.

Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na waandamanaji walirusha mawe na kupulizia mapambo ya graffiti kwenye magari ya polisi.

Mashuhuda walieleza kuwa vurugu hizo zilianza siku ya Jumanne jioni, wakati mamia ya watu walipofika katika eneo ambalo tukio lilitokea, Jumatatu jioni.

Waratibu walijaribu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na kuzingatia masharti ya kukaa mbalimbali, waandamanaji waliimga “siwezi kupumua na ingeweza kuwa mimi”.

Mmoja wa waandamanaji, Anitha Murray aliliambia gazeti la Washinton Post: “Inaogopesha kuwa hapa wakati wa janga la corona, lakini kwa nini nijiweke mbali?”

Kundi la mamia ya watu baadae waliandamana mpaka kwenye idara ya polisi, ambapo maofisa waliohusika na kifo hicho walikuwa wakifanya kazi.

Mtu mmoja alikiambia chombo cha habari cha CBS: “Hii ni mbaya sana. Polisi lazima watambue kuwa hali hii wameitengeneza wenyewe.”

Polisi walisema kuwa mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi lakini taarifa za kina hazijatolewa kuhusu tukio hilo.

Maofisa wanne wa polisi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani wamefutwa kazi kufuatia kifo hicho ambaye alikuwa amekamatwa na kuonekana akizuiliwa chini kwa kushikwa shingo.

Ofisa Mkuu wa Polisi katika jimbo hilo, Medaria Arradondo alisema kwamba maofisa hao wanne sasa “sio wafanyakzi wa kikosi hicho”.

Kanda ya video inaonesha, mtu huyo kwa jina George Floyd, akilia na kuwaambia maofisa hao weupe “siwezi kupumua”.

Kisa hicho kinafanana na kile cha Eric Garner, mtu mweusi aliyefariki akikamatwa na polisi mjini New York mwaka 2014.

Shirika la ujasusi nchini Marekani (FBI) lilisema litachunguza kisa hicho cha Minneapolis kilichofanyika Jumatatu jioni.

Maofisa wa polisi wa Minnesota walisema kwamba Floyd mwenye umri wa miaka 46, ambaye alikuwa anafanya kazi kama ofisa wa usalama katika mkahawa mmoja alifariki akifanyiwa matibabu kufuatia malumbano na maofisa wa polisi.

Siku ya Jumanne, Meya Jacob Frey alithibitisha kwamba maofisa hao wanne waliohusishwa na kisa hicho wamefutwa kazi. 

Katika mkutano na vyombo vya habari mapema, a Frey alikitaja kisa hicho kama cha kushangaza.

“Ninaamini kwamba kile nilichokiona ni kitendo cha makosa kwa kiwango chochote kile. Kuwa mtu mweusi nchini Marekani hakustahili kuwa hukumu ya kifo,” alisema.

Ni madai ya hivi karubuni ya unyanyasaji unaotekelezwa na maofisa wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi.

Visa maarufu vya hivi karibuni vinashirikisha afisa mmoja wa eneo la Maryland ambaye alimpiga risasi mtu mmoja akiwa ndani ya gari la kupiga doria.

Kisa hicho cha Minneapolis kilianza baada ya ripoti kwamba mteja mmoja alikuwa anajaribu kutumia noti bandia ya dola 20 katika duka moja.

Ofisa huyo alimuona mshukiwa akiwa ndani ya gari lake, mtu huyo alikataa kukamatwa kulingana na maofisa wa polisi.

Waliambiwa kwamba mtu huyo ambaye hajatambulika alikuwa ameketi juu ya gari la rangi ya buluu na alionekana kana kwamba ametumia kishawishi fulani.

Baada ya kuagizwa kuondoka na kusimama kando ya gari hilo, jamaa huyo alikataa kukakamtwa lakini maofisa walifanikiwa kumfunga mikono yake kwa pingu na akaonekana kana kwamba alikuwa anaugua tatizo la tiba, taarifa hiyo iliongezea.

Katika kanda hiyo ya dakika 10 iliochukuliwa na shahidi, mtu huyo aliwekwa ardhini na ofisa huyo na katika wakati mmoja alisikika akisema ”musiniue”.

Shahidi mmoja alisikika akimwambia ofisa huyo kuondoa goti lake katika shingo ya mshukiwa huyo, akidai kwamba alikuwa hayumbi.

Mwengine alisema pua yake inatoka damu, huku mwengine akiomba ”ondoka katika shingo yake”.

Mtu huyo anaonekana ametulia kabla ya kuingizwa katika ambulansi na kuondoka naye.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles