23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KICHEKO NA FURAHA TELE KWA AMINEX, SOLO OIL

Na Mwandishi Wetu

BONDE la Mto Ruvuma linaendelea kuthibitisha kuwa lina uwezo mkubwa wa kuwa na gesi asilia na hata mafuta ya petrol, kufuatia kuongezeka uwezekano kwa kiwango kikubwa cha mara tatu kuliko ilivyodhaniwa hapo awali kufuatia ugunduzi na tathmini mpya.

Zamani eneo hilo linalojulikana kiuziduaji kama Ntorya, lilikisiwa  kuwa na hazina ya gesi ya kiasi cha futi za ujazo bilioni (bcf) 186 ya 2C ikitokea kwenye ujazo wa bilioni70.

Mapitio mapya yameonesha kushamiri kwa gesi asilia katika 3C kama ilivyoainisha na huyu mbia mdogo Solo Oil, lakini ni ongezeko la asilimia 230 na kufikia  bcf 766 kutoka 232 kama ilivyoainishwa na Meneja Mradi na Mwendeshaji wa Ntorya, Aminex ambaye ameonesha kukua kwa hazina hiyo.

Kwenye kisima kilichochimbwa mapema mwaka huu katika Ntorya -2 kwenye visima viwili hivyo, vinaonesha kwa pamoja na mwenendo wa kutia tumaini kutoka kwenye vyanzo hivyo vilivyoko nchi kavu na  kuimarisha imani kwa vile Ruvuma ni bonde, basi uwezekano wa kuweko mafuta kuwa ni mkubwa zaidi  bila kuzingatia eneo kubwa lililosalia kuchunguzwa lililoko pembeni ya eneo husika kwa makisio hayo ambalo lina mwelekeo mzuri zaidi.

Kwa kifupi makisio ya ugunduzi huu mpya unaonesha uwepo wa bcf 466 ya gesi kiwango cha chini kilichopo mahali (GIIP) kuongezeka kutoka  ya awali  ya bcf 153.

Makisio mapya yanaanzia bcf 62  katika mfumo wa kizamani wa P90 hadi trilioni 1.13 katika  mfumo mpya wa P10 na kufanya eneo hilo kuwa muhimu kwa uchumi wa Tanzania na hivyo kufanyiwa mpango wa kuunganishwa katika bomba la Taifa, kwani uzalishaji unaweza kuanzishwa muda si mrefu.

Taarifa kutoka Perth, Australia ambako kampuni hizo mbili kuna makao makuu yake, inaonesha kuwa ni habari njema sana kwa  wadau na wenye hisa huko kwa maelezo ya Mtendaji Mkuu, Jay Bhattacherjee kuwa hazina imeongezeka mara tatu.

Alithibitisha kuwa wako karibu  na Serikali juu ya mwenendo mzima wa mradi na wanataka kuongeza kasi ya  utekelezaji ili kuingiza gesi hiyo kwenye bomba la gesi la Taifa.

Aminex ilisema kuwa iko mbioni kushughulikia kuchimba kisima kingine cha Ntorya 3 na kupanga kuwa kizingatie upatikanaji wa mafuta ya petroli ambayo wana imani kubwa kuweko katika eneo hili na hivyo kupanga kuomba leseni ya miaka 25 ya kuendeleza hali hiyo ya uchimbaji ambayo inatia moyo na kujivunia kisima nchi kavu.

“Upatikanaji huo mkubwa  wa gesi unaifanya pwani ya Tanzania kuwa moto na kuwa na mvuto kwa wawekezaji wanaotafuta mafuta kwani wana imani siku itafika watatoboa mwamba wa mafuta  na kufunga kazi kwa mafanikio na chereko,” alisema ofisa mmoja wa TPDC  jijini Dar es Salaam  na kukataa kutajwa jina kwani si msemaji wa shirika.

Pamoja na Tanzania kuwa na hazina ya gesi asilia ya kiasi cha tcf 57.2, ni kiasi cha tcf 2.7 tu ziko nchi kavu kwenye bonde la Ruvu kiasi cha kilomita 30 magharibi ya Dar es Salaam, kwani nyingine yote iko baharini  katika umbali tofauti na mbali zaidi ni kilomita 120 kwenye bahari kuu.

Katika ubia huo, Aminex ina asilimia 75 na Solo Oil Plc asilimia 25 zote ni za Australia, wanataka kuharakisha uzalishaji baada ya kupata vibali husika kutoka Serikali Kuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles