27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

KICHANGA CHA SIKU TANO CHAFARIKI KWA KUKEKETWA

ukeketaji+pic

Na SAFINA SARWATT- MOSHI

MTOTO mchanga wa siku tano amefariki dunia baada ya kufanyiwa kitendo cha ukeketaji na bibi yake aliyejulikana kama Longida Naingola mkazi wa Kijiji cha Naibera, wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, kichanga hicho kutoka kabila la Wamasai kilifanyiwa kitendo hicho cha kikatili Desemba 30, mwaka jana katika Kijiji cha Naibera, wilayani Simanjiro.

“Mtoto alizaliwa Desemba 25, 2016 na Desemba 30, 2016 saa 4:00 asubuhi, bibi huyo alimkeketa na baada ya kitendo hicho hali ya mtoto ilikuwa mbaya kutokana na kutokwa na damu nyingi sehemu zake za siri,” alisema Mutafungwa.

Mutafungwa alisema ilipofika Januari 11, 2017 mtoto huyo alifikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC akiwa na mama yake mzazi, Fatina Joshua (14).

Alisema baada ya kufikishwa hospitalini hapo madaktari waliompokea walimkagua na kukuta mtoto huyo akiwa ameharibika vibaya sehemu zake za siri na ilipofika Januari 13, mwaka huu alifariki dunia.

Kamanda Mutafungwa, alisema baada ya kupata taarifa hiyo waliwatafuta watuhumiwa na kumkamata bibi pamoja na mama wa kichanga hicho.

Alisema mwili wa kichanga hicho umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC huku uchunguzi ukiendelea ili kuchukua hatua zaidi za kisheria.

Aidha, Kamanda Mutafungwa alisema jeshi hilo pia linaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Manyara kutokana na tukio hilo kufanyika huko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles