24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kibonde apandishwa kortini, adhaminiwa

Mtangazji maarufu wa redio nchini, Ephraim Kibonde
Mtangazji maarufu wa redio nchini, Ephraim Kibonde

MANENO SELANYIKA NA CHRISANTA CHRISTIAN, DAR ES SALAAM

WATANGAZAJI maarufu wa redio nchini Ephraim Kibonde (42) na Gadner Habashi (41), jana walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la kutotii amri halali ya polisi wa usalama barabarani.

Katika shtaka la kwanza, Wakili wa Serikali, Salum Mohamed alidai mbele ya Hakimu Aniceta Wambura kuwa washtakiwa wote walitoa lugha chafu kwa askari.

Wakili Mohamed alidai washtakiwa hao walimtukana SGT Sylivester mwenye namba E 884 matusi ya nguoni katika Kituo cha Polisi Oysterbay, Agosti 9, mwaka huu, jambo ambalo lingeweza kuhatarisha amani.

Alisema kosa hilo linakwenda kinyume na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shtaka la pili linamuhusu mshtakiwa wa kwanza peke yake, Kibonde ambapo amedaiwa kutotii amri ya polisi E.4190 CPL Sweetbert tarehe hiyo hiyo katika eneo la Bamaga, ambaye alimtaka asimamishe gari alilokuwa akiendesha lenye namba za usajili T. 759 CPM Toyota aina ya Brevis na kuamua kukimbia.

“Mshtakiwa baada ya kusababisha ajali askari alikuomba kuwa ugeuze gari ulilokuwa ukiendesha na ulikataa kisha kukimbia hadi eneo la Ubungo Mataa ndipo ulikamatwa,” alidai Salum.

Washtakiwa walikana makosa hayo na upelelezi wa shauri hilo tayari umekamilika ambapo Hakimu Wambura alidai kuwa kwa mujibu wa sheria mashtaka yao yanadhaminika hivyo aliwataka walete wadhamini wawili kwa kila mmoja watakaoweka saini ya maandishi ya Sh. milioni 5.

Wakati huo huo, mshtakiwa Kibonde, alipandishwa tena kizimbani katika mahakama hiyo akikabiliwa na makosa mawili likiwemo la kuendesha gari barabarani akiwa amelewa.

Katika shtaka la kwanza, mbele ya Hakimu Aniceta Wambura, Wakili wa Serikali Ramadhani Mkimbu, alidai kuwa Agosti 9 mwaka huu eneo la Makumbusho, Kibonde akiendeha gari lenye namba za usajili T. 759 CPM Toyota Brevis aligonga gari nyingine yenye namba za usajili T 960 CBB aina ya Hyundai Tucson kisha kusababisha uharibifu.

Katika shtaka la pili mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa la kuendesha gari hilo akiwa katika hali ya ulevi ambapo baada ya kupimwa alionekana ana ulevi wenye kipimo cha ujazo wa mililita 190.9 kitendo ambacho ni kinyume na sheria za usalama barabarani.

Mshtakiwa alikana makosa yake na upelelezi umekamilika. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 10, mwaka huu na yupo nje kwa dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles