33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kibajaji amtaka mke wa Mtikila kumshtaki Zitto Kabwe kwa kuiba ‘style’ ya mumewe


Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde maarufu Kibajaji, amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, kuacha kutumia siasa kama zilizokuwa zikifanywa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha DP, marehemu Mchungaji Christopher Mtikila za kushinda mahakamani kufungua kesi.

Kibajaji amesema hayo leo Jumamosi Januari 19, katika mkutano wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Zitto kuwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ikienda bungeni itapita kwa sababu wabunge wa CCM wengi ni makasuku.

Amesema Zitto akiendelea kufanya siasa ambazo anaendelea nazo atashitakiwa na mke wa Mtikila.

“Zitto sasa hivi anachukua ‘style’ za Mzee Mtikila za kushinda Mahakamani badala ya kushinda kutafuta hoja na watu wake wa Kigoma.

“Yaani yupo ACT Wazalendo lakini akili anazotumia ni za hayati Mtikila, nadhani mke wa Mtikila kama kungekuwa na sheria ya kusimamia stahiki za mumewe ana uwezo wa kumshtaki Zitto ili aweze kumlipa fidia kwa kutumia jina la mumewe yaani Zitto Mtikila,” amesema.
Kuhusu kauli ya Zitto, Lusinde amesema kazi ya bunge si ya kubeza, iwe mbaya au nzuri ndiyo kazi ya Bunge.

“Mimi namuona kama vile siku hizi ametoka kwenye reli kwa sababu hata ukimsikiliza vizuri mimi nadhani ana tatizo kubwa sana.

“Unawezaje kusema sheria hii ikienda bungeni itapita kwa sababu wabunge wa CCM wote ni makasuku wakati bungeni yupo mkewe (Halima Bulembo) na mkwewe (Abdallah Bulembo) yupo sawa kweli huyo, Zitto anapaswa kujitafakari upya kwa sababu anakoelekea anaenda shimoni kabisa,” amesema Lusinde.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles