30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

KHLOE KARDASHIAN APIGWA ‘KIBENDI’

NEW YORK, MAREKANI


MDOGO wake Kim Kardashian, mwanamitindo Khloe Kardashian, amethibitisha kuwa na ujauzito wa miezi minne.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 33, amepwa ujauzito huo na mpenzi wake ambaye ni nyota wa kikapu wa timu ya Cleveland Cavaliers inayoshiriki Ligi Kuu ya NBA nchini Marekani, Tristan Thompson mwenye umri wa miaka 26.

Mtoto huyo atakuwa wa kwanza kwa wawili hao, lakini atakuwa wa pili kwa Thompson ambapo mtoto wake wa kwanza anajulikana kwa jina la Prince Thompson, aliyezaliwa Desemba 12, mwaka jana na mrembo Jardan Craig.

“Nina furaha kubwa kutarajia mtoto na mpenzi wangu Thompson, nadhani huyu ni mwanamume sahihi kwangu pamoja na familia kwa ujumla, amekuwa mlinzi wa familia yangu, maneno yake yanasimama popote na familia kwa ujumla inampenda sana,” alisema Khloe.

Mbali na Khloe kutarajia mtoto, pia familia hiyo ya Kardashia inatarajia mtoto mwingine kutoka kwa mdogo wao Kylie Jenner mwenye umri wa miaka 20, anayetoka na rapa Travis Scott.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles