Khloe hana mpango wa kuongeza mtoto

0
668

LOS ANGELES, MAREKANI

MREMBO kutoka familia ya Kardashian, Khloe Kardashian, amefunguka na kusema kwa sasa hajafikiria kuongeza mtoto wa pili kwa siku za hivi karibuni.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 34, tayari ana mtoto mmoja ambaye alizaliwa miezi nane iliyopita akijulikana kwa jina la True Thompson huku baba yake akiwa ni nyota wa kikapu wa timu ya Cleveland Cavaliers.

“Naipenda sana familia yangu, nampenda mwanangu True na ananifanya nionekana kuwa nimekamilika katika maisha ya familia.

“Kwa sasa sijafikiria kuongeza ukubwa wa familia yangu, nadhani muda bado, sidhani kama kuongeza mtoto mwingine kutanifanya nionekane kuwa nimekamilika zaidi, hapana muda wa kupanga haujafika,” alisema mrembo huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here