KHLOE AHAMIA KWA THOMPSON KULEA UJAUZITO

0
302

NEW YORK, MAREKANI


HATIMAYE mwanamitindo Khloe Kardashian ameamua kufungasha mizigo yake na kuhamia kwa mpenzi wake, Tristan Thompson, kwa ajili ya kutazamia ujauzito wake.

Thompson ni nyota wa mchezo wa kikapu wa timu ya Cleveland Cavaliers, inayoshiriki Ligi Kuu ya NBA nchini Marekani. Mwezi uliopita wawili hao walithibitisha kuwa wanatarajia mtoto mapema mwakani.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Thompson ameweka wazi kuwa, tayari mpenzi wake ambaye ni mdogo wake Kim Kardashian, amehamia kwake ili waweze kulea ujauzito wao.

“Hatimaye yupo nyumbani kwangu tunaishi wote kwa sasa, hii inaonesha wazi kuwa tunatarajia kuongeza ukubwa wa familia yetu, tunaamini hakuna mapenzi ya kukaa mbali, itakuwa ni kuongopeana,” aliandika Thompson.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here