23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi za Corona Afrika zapindukia 40,000

 ADDIS ABABA, ETHIOPIA

IDADI ya kesi za ugonjwa wa Covid-19 (Corona) zilizothibitishwa katika nchi za Afrika kufikia jana imepindukia 40,000, kutoka 39,018 iliyoripotiwa Ijumaa iliyopita.

Hayo ni kwa mujibu wa takwimu mpya za Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) ambazo zinaonyesha kuwa, idadi ya vifo vilivyosababishwa na Covid-19 barani Afrika imefikia 1,689.

Kituo hicho kimesema kufikia juzi Jumamosi kesi 40,746 za maambukizi ya virusi vya Corona zilikuwa zimethibitishwa barani Afrika, lakini habari njema ni kwamba wagonjwa zaidi ya 12,200 wa Covid-19 wamepata afueni barani humo.

Hadi kufikia jana, idadi rasmi zilizokuwa zimetangazwa kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki; ni Tanzania wagonjwa 480, Kenya wagonjwa 435 na Uganda wagonjwa 88 wa corona. Walioaga dunia kwa corona nchini Tanzania kufikia sasa ni watu 16 na Kenya ni watu 22.

Nchini Rwanda idadi ya watu walioambukizwa corona hadi sasa ni 243 huku idadi wa wagonjwa wa corona Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakifikia 674, kati ya hao, 33 wameshafariki dunia na 75 wengine wamesharejea katika hali nzuri za kiafya.

Virusi vya corona vinaenea kwa kasi barani Afrika na nchi zilizoathiriwa zaidi ni zile za Kaskazini mwa bara hilo za Misri, Morocco, Algeria pamoja na Afrika Kusini.

Nchini Somalia, Meya wa Mogadishu amesema anaona kua ugonjwa wa Covid-19 umeua watu zaidi ya 500 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita katika mji mkuu huo wa Somalia pekee.

Omar Mohamud Filish alikosoa takwimu za vifo na maambukizi ya corona zinazotolewa na serikali akisisitiza kuwa haziakisi hali halisi katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Alisema mji mkuu huo wa Somalia unarekodi kati ya vifo 19 na 49 vya corona kila siku na kwamba, kuanzia Aprili 19 hadi Ijumaa ya juzi, jiji hilo lilikuwa limenakili kwa karibu vifo 500 vya wagonjwa wa Covid-19. Wataalamu wa afya na wachimbaji makaburi nchini humo waliohojiwa na gazeti la The Gurdian la Uingereza walieleza wasi wasi kutokana na ongezeko la idadi ya watu wanaozikwa kila siku nchini Somalia.

Dereva mmoja wa gari la wagonjwa alisema binafsi huwa anabeba maiti 18 karibu kila siku kwa ajili ya kwenda kuzikwa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kinyume na ilivyokuwa huko nyuma.

Hii ni katika hali ambayo, Fowziya Abikar Nur, Waziri wa Afya wa Somalia juzi alitangaza kuwa nchi hiyo ilirekodi kesi mpya 70 za corona, na kupelekea idadi ya waliombukizwa virusi hivyo hadi sasa nchini humo kufikia 671.

Aidha alisema watu watatu waliaga dunia kwa ugonjwa huo na kufanya idadi ya wahanga wa corona mpaka sasa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kufikia 31.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles