24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Mbowe, viongozi Chadema yamuibua Nyalandu

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wenzake nane wa chama hicho.

Nyarandu alifika asubuhi, alifanikiwa kuingia mahakamani saa tatu na nusu asubuhia na washtakiwa walipofika alisalimiana na Mbowe na Matiko waliopo gerezani kwa miezi takribani mitatu sasa tangu walipofutiwa dhamana.

Mbowe aliyekuwa anaumwa mara ya mwisho lakini leo ameweza kufika mahakamanj kusikiliza kesi ya kina Mbowe.

Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina baada ya Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, Wilbard Mashauri kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alidai kesi ilikuja kwa kutajwa wanaomba tarehe nyingine na Mahakama ilipanga kuitaja tena Februari 14 mwaka huu.

Mbali Mbowe, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji na Mchungaji Peter Msigwa.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari mosi na 16, mwaka 2018, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles