24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Malinzi kusikilizwa siku tatu mfululizo


KULWA MZEE – DAR ES SALAAM 

KESI inayomkabili, aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wanne inatarajia kusikilizwa mfululizo siku tatu kuanzia Januari 16 mwakani.

Kesi hiyo ilitakiwa kuendelea jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri lakini ilikwama kwa sababu shahidi wa Jamhuri kapata matatizo ya kifamilia.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leonard Swai amedai shahidi waliyemtegemea kapata matatizo ya kifamilia aliomba kesi iahirishwe.

Akijibu Wakili wa utetezi, Richard Rweyongeza alidai Jamhuri walitakiwa kuwa na mashahidi wawili akaomba hiyo hali ya kuwa na shahidi mmoja isijirudie.

Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza hoja zote aliahirisha kesi hadi Januari mbili kwa kutajwa na Januari 16, 17 na 21 mwakani kusikilizwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo mbali na aliyekuwa rais TFF, Jamal Emil Malinzi (57) wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine (46) na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga(27).

Meneja wa  Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335 na Sh 43,100,000.

Malinzi,  Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku wenzao Zayumba na Frola wapo nje kwa dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles