31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KESI DHIDI YA NAIBU JAJI MKUU KENYA YASIMAMISHWA

 

NAIROBI, KENYA


Mahakama Kuu ya Kenya imesimamisha uendeshaji wa kesi ya ufisadi dhidi ya Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu.

Hatua hiyo, inafuatia ombi la Mwilu katika mahakama hiyo kuwa asijibu mashtaka ya ulaghai, utumiaji mbaya wa madaraka na kukwepa kulipa kodi, kesi iliyowasilishwa dhidi yake juzi na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma.

Alikamatwa Jumanne katika majengo ya Mahakama ya Juu i na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu ambapo baadaye aliachiliwa huru kwa dhamana.

Kupitia wakili wake, Okongo Omogeni, Mwilu ameiambia Mahakama Kuu jana asubuhi kwamba kesi hiyo iliyowasilishwa dhidi yake ina hila na ni njama dhidi yake.

Katika ombi lake mahakamani, alikuwa amewashtaki Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Idara ya Uchunguzi wa Jinai, Mwanasheria Mkuu na Hakimu Mkuu anayeangazia kesi za ufisadi.

Mahakama ya Juu sasa imeamua kusitisha kesi ya uhalifu inayomkabili Mwilu kukisubiriwa kuamuliwa masuala ya kikatiba yanayotokana na ombi alilowasilisha.

Jaji Chacha Mwita wa Mahakama Kuu ameeleza ombi hilo la Mwilu linazusha masuala makuu.

Naibu Jaji Mkuu huyo anakabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo kutumia vibaya madaraka yake, na kutolipa ushuru.

Inadaiwa kuwa jaji huyo alikiuka sheria ya uongozi na maadili kwa kupokea mkopo binafsi wenye thamani ya dola 120,000 kutoka kwa Benki ya Imperial.

Mwilu hata hivyo amejitetea kwa kusema mkopo huo ulitokana na makubaliano ya kibiashara.

Mahakama hiyo imeamua sasa kuna masuala ya kutathminiwa kikatiba kubaini iwapo makubaliano ya kibiashara baina ya mtu na taasisi ya kibiashara yanaweza kutazamwa kama mashtaka ya uhalifu.

Kwa sasa kesi hiyo ya uhalifu imesimamishwa hadi Oktoba 9.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles