25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KENYATTA: Watu 14 wameuwawa kwenye shambulizi

Na Anna Potinus – Dar es Salaam

Rais Uhuru Kenyatta amesema watu 14 wamefariki na wengine 700 wameokolewa na vyombo vya ulinzi na usalama kwenye shambulio la kigaidi katika hoteli ya kifahari ya DusitD2.

Kenyatta ameyasema hayo leo alipokuwa akililitubia Taifa juu ya shambulio la kigaidi lililotokea January 15, 2019 katika Hoteli ya kifahari ya DusitD2 iliyopo eneo la Riverside jijini Nairobi.

Amesema kuwa tayari opereshini imekamilika na washambuliaji wote wameshauwawa.

Rais ameongeza kuwa, “Sisi kama taifa tunaomboleza na tunawaombea majeruhi wapone haraka lakini pia tunaendelea kudumisha usalama nchini,”.

Aidha Rais Kenyatta amesema nchi yao ni ya amani na ina sheria na kwamba hawataweza kusahau wale waliohusika na shambulizi hilo na kwamba tayari ameshafanya mkutano na asasi za kiusalama juu ya namna ya kuwashughulikia magaidi hao.

Pia amesisitiza kuwa nchi iko salama kwa sasa na kuwataka wageni na wenyeji waendelee kusukuma gurudumu la maisha huku akiwaasa wakenya kusambaza ujumbe wa kutiana moyo katika mitandao ya kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles