KENYATTA APUNGUZA KODI YA MAFUTA

0
464

NAIROBI, KENYARais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametangaza uamuzi wa kukubali kupunguza bei ya bidhaa ya mafuta kutoka asilimia 16 hadi 8, ikiwa ni njia mojawapo ya kuwapunguzia gharama wananchi wake.

Akihutubia taifa hilo kwa njia ya runinga, Rais Kenyata amesema kuwa, amesikia kilio cha Wakenya kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa muhimu na usafiri.

Mbali na kupunguza kodi ya mafuta, Rais Kenyatta amepunguza gharama za mapokezi, burudani, mafunzo na mikutano, na usafiri katika nchi za nje.

Hata hivyo amependekeza kuongezwa fedha katika idara za utekelezaji wa sheria na hivyo kuweza kukusanya kipato zaidi kupitia mahakama nchini.

Mapendekezo yote hayo ya Rais Kenyatta yanasubiri kuidhinishwa bungeni wakati wa kikao maalumu Septemba 18, mwaka huu.

Hata hivyo, bado Serikali ya Kenya ina kazi kubwa ya kulishawishi Shirika la Fedha Dunia, IMF na kujua wapi itakapopata zaidi ya dola milioni 90 kuziba pengo katika nakisi ya bajeti.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kuorodhesha uwezo wa mataifa kukopa, Moody limesema Kenya inakabiliwa na ongezeko la deni la taifa, ambalo kwa sasa linakadiriwa kuwa limefika asilimia 58 ya pato la jumla la nchi.

Kwa sasa wananchi wa Kenya wamejawa na furaha, huku kila kona ukiwakuta watu wakizungumzia uamuzi huu wa Rais Uhuru Kenyatta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here