31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KENYA YAPOTEZA BILIONI 4/- KWA UDUKUZI

NAIROBI, Kenya

MWANAMUME moja ameshtakiwa kwa tuhuma za kudukua mfumo wa kifedha wa Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA).

Udukuzi huo unadaiwa kusababisha mamlaka hiyo kupoteza jumla ya Sh bilioni 4 za Kenya ambayo ni sawa na Dola za Marekani milioni 39.

Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, Alex Mutunga Mutuku, alishtakiwa makosa ya kutekeleza ulaghai kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa  Mutuku alikuwa sehemu ya mtandao mkubwa wa watu waliokuwa wakiiba pesa kutoka kwa taasisi na kampuni kubwa nchini humo.

Alidaiwa kutekeleza makosa hayo kati ya Machi 2015 na Machi mwaka huu.

Gazeti la Standard lilisema kuwa, wakili wa upande wa mashtaka Edwin Okello aliambia mahakama: "Sakata hii ni kubwa na inahusisha hata watu walio nje ya nchi” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles