KENYA WALIA NA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA

0
470
3d rendered and waving flag of kenya
Nairobi, Kenya

Serikali ya Kenya, kupitia tume ya Nishati imeidhinisha asilimia 16 ya tozo la kodi kwa bidhaa za mafuta nchini humo.

Hivi sasa lita moja ya mafuta ya petroli inauzwa kwa takriban shilingi 127 huku dizeli ikiuzwa kwa shilingi 115 na mafuta ya taa shilingi 96 za Kenya, hii ikiwa ni ongezeko la shilingi 14 za Kenya.

Hata hivyo, baadhi ya raia wameonesha kutoridhishwa na hatua hiyo kupitia mitandao ya kijamii, wamekuwa wakitoa shinikizo kwa rais Uhuru Kenyatta na serikali yake kuchelewesha kutia saini marekebisho hayo ya sheria yatakayochelewesha kuidhinishwa kwa tozo hilo la ushuru.

Aidha, athari zinazotarajiwa ambazo baadhi zimeanza kudhihirika kutokana na kupandishwa kwa bei ya mafuta ni pamoja na kupanda kwa nauli za usafiri wa umma.

Lakini pia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu wakati wakulima na wachuuzi wakiathirika kwa upande wao kwa gharama kubwa ya kusafirisha mazao yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here